Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 za bara la Afrika zitakazoshiriki katika tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ linalotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa katika mji wa ‘Cherbourg-Octeville’ mwezi Julai mwaka huu.
Tanzania inashiriki tamasha hilo la kihistoria kwa mara ya kwanza ambapo itapata fursa ya kutangaza utamaduni wake na vivutio vya utalii vya mambo ya kale hivyo kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha hilo Jijini Dar es Saalam jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, alisema tamasha hilo litatoa fursa pana kwa nchi kutangaza vivutio vyake ikiwemo vile vya Zamadamu.
“Kimsingi tamasha hilo linatarajiwa kutoa fursa kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini, kila nchi itapewa banda lake la kuonyesha vivutio vyake , Tanzania naamini inakuwa na vivutio vingi vyenye kupendeza watalii kama vile Zinjathropus, Ngoma za makabila mbalimbali pamoja na nyimbo.
“Baada ya tamasha hilo, kutakuwa na ongezeko kubwa la watalii nchini na ninaamini hata zile nchi ambazo hazina rekodi nzuri ya kuja Tanzania kwa wingi zilizopo Bara la Asia zitaanza kuja,’’. alisema Dkt. Kigwangalla.
Alisema tamasha hilo linalotarajiwa kuhusisha takriban nchi zote za bara la Afrika, zaidi limelenga kutangaza tamaduni na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika mataifa yote yatakayoshiriki huku likitajwa kuwa tamasha bora na kubwa la utalii pengine kuliko matamasha mengine yote kutokana na kila nchi kujitokeza kuonyesha vivutio vinavyopatikana katika mataifa yao.
“Tanzania tunavyo vivutio mbalimbali tunavyotarajia kwenda kuvionyesha katika tamasha hilo, ukiacha vivutio vya mambo kale, tuna bonde la Olduvai Gorge na mengineyo, tunayoamini kuwa kupitia tamasha hilo tutaweza kuyatangaza na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini” alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo alisema baada ya kukamilika kwa tamasha hilo, Septemba mwaka huu hapa nchini kutakuwa na tamasha la ‘Urithi wa Mtanzania’ linalotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza na litakuwa likifanyika kila mwaka kuadhimisha urithi wa Mtanzania. Alisema tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha mwezi mzima, pia litatoa fursa kwa kila wilaya kutangaza vivutio vyake, huku akizitaka kila wilaya kujiandaa na tamasha hilo, litakalotoa fursa pia kwa mikoa na wilaya hizo kukuza utalii wa maeneo yao.







Related
Published by Mbilinyi-Wildlife
Conservation has always been a major part of my life. Growing up I revered leaders like famous oceanographer Jacques Cousteau and conservationist Jane Goodall, and I dreamed of becoming a swayful wildlife conservationist one day. Some of my fondest memories are of exploring the Amani forests with my college's friend, learning about both the awesome power of nature the threats to its well being.
I ultimately pursued a career in wildlife management at college of African wildlife management -Mweka and my friends too become a conservationists. Together, we founded Saviours of Wildlife with our slogan that Who pays for wildlife and who benefits?.
I recognize there are many conservation organizations doing incredible work on behalf of our planet and the many species who call it home.
I wanted to create an organization that complemented and collaborated with these organizations, so we chose to focus on protecting lesser-known endangered species.
My speech
If there’s one thing we know about life on Earth, it is that all of our diverse animals, plants, soil structures and waterways are interconnected in complex ways, many of which we cannot fully understand. In order to maintain ecological balance, we need to focus on all of the puzzle pieces–and this is becoming harder to do as we lose more and more species to climate change and human activity.
Saviors of wildlife focuses on lesser-known species because they are our early-warning signals for larger issues facing the ecosystem. For example, amphibians have a tremendous impact on their environment. They are not the face of environmental conservation in the same way as elephants,rhinoceros or gorillas, but because of their size and genetic makeup, these creatures are much more sensitive to climate change.
For example, saviour of wildlife is working to save amphibians, reptiles but also supporting efforts of conserving big wildlife like Rhino, giraffe and elephants through conservation education and capacity building to wildlife practititoners.
Saviours of wildlife is also working to save the world’s most endangered marine mammals. Only about 30% are left in the wild due to them becoming entangled in gill nets set for illegal fishing activities.The marine creatures are the most endangered Species.
Our planet is facing a biodiversity crisis. Last month , I was fortunate to share comment with Jane Goodall to discuss this critical issue. She reminded the word that she spoke to me 5 years ago “don’t forget, every single one of you makes a difference every single day.”
As we sit on the brink of losing thousands of more species, throwing our future into jeopardy, I am now asking you to make smart decisions .Please join us in reversing this crisis and making our collective future more secure contact
Brighton Mbilinyi, saviours of wildlife,college of African wildlife management.
brightonfrancis91@gmail.com +255756 525739
View all posts by Mbilinyi-Wildlife