​NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE  KUVAMIA  HIFADHI. 

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi wanaozunguka hifadhi za misitu katika wilaya ya Kisarawe kuzingatia mipaka iliyowekwa pamoja na matumizi ya ardhi ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baina ya wananchi na serikali.Hasunga alisema jana kwenye ziara aliyoifanya alipotembelea Kiwanda cha Caoline, pamoja na msitu wa hifadhi Kazimzumbwi na Pugu.Alisema serikali haitakubali kuona maeneo ya hifadhi yanavamiwa ovyo na wananchi ama mifugo kuachiliwa bila utaratibu maalum.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kukuza sekta ya utalii. Wataalii wengi wanapenda kuona misitu. Hii ni sehemu ya utalii,” alisema.Aliwataka Kisarawe kuangalia vivutio walivyonavyo ili kuboresha katika maeneo hayo kwa ajili ya kuvutia utalii.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Misitu Kisarawe, Mathew Mwanuo alisema wilaya hiyo ina misitu minne ya hifadhi ya serikali Kuu ambayo ni Ruvu Kusini, Masanganya, Pugu na Kazimzumbwi.

Alisema msitu wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na watu kutoka maeneo mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam.

“Msitu huu ulikuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014. Hata hivyo wavamizi hao waliendelea kuvamia kwa nyakati tofauti hadi mwaka huu,” alisema.Alisema walianza kuwaondoa mwishoni mwa Agosti mwaka huu, Kamati ya Ulinzi na Usalam ya wilaya ya Kisarawe kwa kushirikiana na maofis wa Wakala wa Huduma za misitu

 Tanzania walianza kutembelea eneo la msitu kuangalia uvamizi na uharibifu uliofanyika katika Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi ikiwa ni pamoja na kuona ukubwa wa uharibifu na namna ya kutekeleza zoezi.

Leave a Reply