Siku ya wanyamapori duniani.(world wildlife day)

Leo ni siku ya uhifadhi wa wanyamapori duniani. Siku hii huadhimishwa kila tarehe 4 ya mwezi Disemba. Mara ya kwanza iliadhimishwa mwaka 2012. Siku hii inalenga kupaza sauti juu ya umuhimu wa kuhifadhi wanyamapori wetu ambao hata vitabu vya Mungu vinatuelekeza kuwahifadhi. Leo basi kata shauri kuchukua hatua zitakazosaidia kuwahifadhi wanyamapori mfano kujieleimisha juu ya umuhimu wa wanyamapori kwa uchumi wa nchi na mazingira, kutoa elimu ya uhifadhi kwa marafiki na ndugu na jamii yako na kuripoti kila uonapo vitendo vyovyote vinavyotishia usalama wa wanyamapori. Usikae kimya paza sauti na anza leo

Leave a Reply